Tunatupa karata yetu ya kwanza ya ASFC Leo

KIkosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex kuikabili Tembo FC katika mchezo wa hatua ya pili ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Tembo ambayo ni timu ya Jeshi kutoka Tabora ipo daraja la pili na hatujawahi kukutana nayo na hii ni mechi yetu ya kwanza.

Ingawa ni timu ndogo na haina nyota wenye majina makubwa lakini hatuta wadharau na tutaingia uwanjani kwa tahadhari zote ili tutinge hatua inayofuata.

Mechi ya kwanza ya Pa Jobe, Fred Michael na Balua…..

Washambuliaji wetu wa Kimataifa Pa Omar Jobe na Freddy Michael wataonekana kwa mara ya kwanza katika mchezo wa leo.

Pia kiungo mshambuliaji Edwin Balua nae ataonekana kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi chetu kutokana na kujiunga na timu baada ya kurejea kutoka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Wengine watatu walionekana Kombe la Mapinduzi

Wachezaji Saleh Karabaka, Babacar Sarr Ladack Chasambi ambao nao tumewasajili katika dirisha dogo la usajili wao waliwahi kufika na walishiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER