Tunatupa karata yetu ya kwanza Ligi ya Mabingwa Leo

Kikosi chetu leo kitaanza kampeni ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na Power Dynamos katika mchezo utakaopigwa katka Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola; Zambia.

Sisi ni miongoni mwa timu chache ambazo hazikuanza hatua ya awali hivyo leo ndio mechi yetu ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robertinho aelezea mipango ya timu

Kocha Mkuu, Roberto Olivier ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa tutaingia kwenye mchezo wa leo kwa lengo la kucheza soka safi na kushinda.

“Simba ni timu kubwa na mara zote tunawaza vitu vikubwa. Tunahitaji kufanya vizuri kwenye michuano hii msimu huu na hii ndio mechi yetu ya kwanza leo.

“Tutaingia kwenye mchezo wa leo kwa lengo la kucheza kandanda safi pamoja na kupata ushindi,” amesema Robertinho.

Phiri afunguka nae

Mshambuliaji, Moses Phiri amesema kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo wa leo na yupo tayari kujitoa kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki wetu.

Phiri ameongeza kuwa tumejiandaa pia kisaikolojia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Power Dynamos lakini tupo tayari kuwakabili.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo wa leo, tunafahamu itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga na tupo tayari kuhakikisha tunashinda,” amesema Phiri.

Kuhusu mashabiki waliosafiri kutoka Tanzania kuja kutupa sapoti Phiri amesema “ni jambo kubwa wamelifanya na wametutia moyo, tupo tayari kuwalipa furaha.”

Chama aweka historia

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama ndiye mchezaji pekee ambaye amezichezea timu zote mbili za leo.

Tuliwafunga 2-0 Agosti 6,2023

Zimepita siku 41 tangu tulivyowafunga Power Dynamos mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye kilele cha Simba Day Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER