Tunataka taji letu la VPL leo

Alama tatu dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga kwenye mchezo wa leo zitatufanya kutawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kwa mara ya nne mfululizo na ndiyo jambo pekee tunalotaka litokee.

Tangu tumeanza msimu lengo letu kuu lilikuwa ni kuhakikisha tunatetea taji letu la ligi na leo ndiyo siku yenyewe ya kufanikisha mpango huo.

Litakuwa ni jambo zuri na la kufurahisha kuchukua ubingwa kwa kumfunga mtani kwa sababu furaha inakuwa maradufu.

Kiufundi maandalizi yamekamilika wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu na yeyote atakayepewa nafasi ya kucheza atakuwa tayari kuipigania nembo ya klabu.

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema mchezo wa Derby mara zote unakuwa na presha kubwa lakini wachezaji wameandaliwa kimwili na kiakili kuikabili hali hiyo ili kutimiza malengo yetu.

“Mechi ya Derby siku zote ni ngumu na ina presha kubwa lakini tumejiandaa kuikabili hali hiyo. Tangu tunaanza msimu lengo letu kuu lilikuwa ni kutetea ubingwa na itakuwa vizuri tukichukua mbele ya mtani leo,” amesema Matola.

TAARIFA YA KIKOSI

Kuelekea mchezo wa leo wachezaji wapo kwenye hali nzuri isipokuwa tutaendelea kukosa huduma ya Ibrahim Ajibu anayesumbuliwa na Malaria pamoja na Jonas Mkude ambaye suala lake la nidhamu bado halijamazika.

MUGALU AREJEA

Mshambuliaji wetu Chris Mugalu ambaye alikosa mechi kadhaa za ligi zilizopita kutokana na kuwa majeruhi amerejea kikosini na yupo tayari kwa mchezo wa leo.

Wiki iliyopita Mugalu alianza mazoezi pamoja na wenzake na kwa sasa yuko fiti na kama benchi la ufundi litaona inafaa linaweza kumtumia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER