Tunashuka tena dimbani kesho

Kikosi chetu kinatarajia kucheza mchezo wa tatu wa kirafiki dhidi ya timu ya Haras El Hodood iliyopanda daraja ya kushiriki Ligi Kuu ya Misri msimu ujao mtanange utakaopigwa katika Mji wa Cairo.

Mchezo huo utapigwa kesho saa 10 Jioni kwa saa za hapa Misri ambapo ni sawa na saa 11 kwa huko nyumbani.

Kocha Mkuu Zoran Maki, amesema mchezo dhidi ya Haras utakuwa na lengo la kuangalia maendeleo ya timu yetu katika eneo la kiufundi na utimamu wa mwili.

Kocha Zoran amesema ameridhishwa na kiwango cha timu katika mchezo uliopita dhidi ya Abo Hamad hasa kipindi cha pili kwani wachezaji walikuwa na kasi tofauti na cha kwanza.

“Mimi ni muumini wa soka la kasi, sitaki mchezaji akae na mpira muda mwingi na sitaki pasi za nyuma, katika mchezo uliopita kipindi cha kwanza wachezaji walikuwa wanakaa sana na mpira na kupiga pasi zisizokuwa na faida

“Lakini kipindi cha pili kasi iliongezeka na wachezaji walikimbia kuelekea mbele ndo maana tukaweza kupata magoli matano ukilinganisha na kipindi cha kwanza ambacho tulifunga goli moja pekee,” amesema Kocha Zoran.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER