Tunashuka Liti leo kuikabili Singida Big Stars

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Liti mkoani Singida kuikabili Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa tunajua tunakutana na timu imara yenye wachezaji bora pamoja na benchi la ufundi lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi.

Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na jana wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Liti kujiandaa na mchezo wa leo.

MGUNDA: TUNAIHESHIMU SINGIDA

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema tunawaheshimu wapinzani wetu Singida Big Stars kutokana na ubora walio nao kwa sasa ndiyo maana tutachukua tahadhari zote.

Mgunda amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo tayari kuhakikisha wanapigania nembo ya Simba kutafuta alama tatu ugenini.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tayari tumefika mkoani Singida wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tunaamini itakuwa mechi ngumu na tutapata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kushinda,” amesema Mgunda.

ZIMBWE JR AWATOA HOFU WANASIMBA

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema ingawa tutakutana na timu ngumu lakini tupo tayari kuhakikisha tunapambana kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Simba ni timu kubwa na tunajua tunaenda kukutana na timu imara kwahiyo tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

KILA LA KHERI SIMBA QUEENS

Wakati huo huo, Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens leo saa moja usiku itashuka dimbani kuikabili Mamelodi Sundowns katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika zinazoendelea nchini Morocco.

Hii ni historia kwa timu kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki kufika nusu fainali hivyo tunaungana na kuwaombea dada zetu ili kufanikiwa kutinga fainali.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SIMBA QUEENS.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER