Tunarejea Ligi Kuu kwa kuikaribisha Ihefu Leo

Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ihefu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunashuka katika mchezo wa leo tukiwa nakumbukumbu nzuri ya kushinda mechi zote tano za ligi tulizocheza tangu msimu wa ligi uanze.

Robertinho afunguka….

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anafahamu mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora walionao lakini tupo tayari kupambania alama tatu.

Robertinho amesema amewatazama jinsi Ihefu wanavyocheza kitimu na kuna muda wanatumia nguvu kitu ambacho kimefanyiwa kazi mazoezini.

Robertinho ameendelea kusema kuwa anawaamini wachezaji wetu ni bora na wapo tayari kucheza soka safi na kushinda.

“Tumerejea kwenye ligi kwa nguvu na tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kupata matokeo chanya kwa kucheza soka safi,” amesema Robertinho.

Chilunda atoa neno…..

Mshambuliaji, Shabani Chilunda amesema kwenye ligi kila mechi ni ngumu ila wao wamejiandaa kuhakikisha tunacheza soka safi na kushinda.

“Mechi itakuwa ngumu, tunaiheshimu Ihefu lakini tumejiandaa vizuri. Kila mchezaji atayepata nafasi atakuwa tayari kuipigania timu kupata ushindi,” amesema Chilunda.

Tuliwafunga bao moja msimu uliopita

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi msimu uliopita tuliibuka na ushindi wa bao moja.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 11 bao hilo pekee lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Pape Sakho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER