Tunakutana na Yanga Mei 28 Kirumba

Ratiba ya mchezo wetu wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga imepangwa kufanyika Mei 28 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezo huo utakuwa kama kisasi kwa kuwa katika mechi zote mbili za msimu huu tulizokutana zilimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Julai 12 mwaka 2020 tulikutana katika mchezo wa robo fainali kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo tuliibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Katika mchezo huo tutahakikisha tunapata ushindi na kutinga fainali ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea taji letu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER