Tunafungua mwaka na Azam

Heri ya Mwaka mpya wa 2022 wanachama, wapenzi na mashabiki wetu popote mlipo duniani. Leo kikosi chetu kinashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam FC kwenye muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Ingawa tunajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu lakini tumejipanga kushinda ili kuwapatia zawadi ya mwaka mpya wapenzi na mashabiki wetu.

Kikosi kipo kamili na wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho jana kujiandaa na mchezo huo na kila atakayepata nafasi yupo tayari kuipigania timu.

KAULI YA KOCHA PABLO

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema mchezo utakuwa mgumu Azam ni timu nzuri na mara zote wamekuwa wakitupa changamoto lakini tumejipanga kuwakabili.

“Mchezo utakuwa mgumu, Azam ni timu nzuri na ina wachezaji bora lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo na kufungua mwaka vizuri,” amesema kocha Pablo.

BOCCO AFUNGUKA

Nahodha John Bocco, amesema maandalizi waliyopata kuelekea mchezo wa leo ni mazuri na watahakikisha wanafuata maelekezo ya mwalimu ili tupate ushindi.

“Kila kitu kiko sawa maandalizi yamekamilika, wachezaji wote tuko tayari. Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Azam ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Bocco.

MECHI ZETU ZILIZOPITA TULIVYOKUTANA

Katika mechi nane tulizotukana na Azam kwenye Ligi Kuu tumeshinda mechi nne na kutoka sare nne. Hii inamaana ndani ya misimu minne hatujawahi kupoteza dhidi ya Azam.

Azam 0-0 Simba (09/09/2017)

Simba 1-0 Azam (07/02/2018)

Azam 1-3 Simba (22/02/2019)

Simba 0-0 Azam (13/05/2019)

Simba 1-0 Azam (23/10/2019)

Azam 2-3 Simba (04/03/2020)

Simba 2-2 Azam (07/02/2021)

Azam 1-1 Simba (15/07/2021)

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. Naipenda Sana timu yang Simba.
    Nashauri kwamba Ni vzr scouting ya usajili iwe makini.
    Pia nawapongeza wachezaji na viongozi kwa kujitolea kwao ili kuhakikisha tunashinda kila mechi.
    Inshallah!

Leave a Reply to Nicholas John Masanja Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER