Tunacheza na St. George Simba Day

Ni rasmi tutacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya St. George kutoka Ethiopia katika kilele cha Tamasha letu la Simba Day litakalofanyika Jumatatu Agosti 8, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

St. George ni Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini humo wakiwa ndiyo mabingwa waliotwaa ubingwa mara nyingi wakifanya hivyo mara 29.

St. George wakiwa na kikosi chao kamili watawasili nchini Jumamosi saa saba mchana ambapo watapata nafasi ya kufanya mazoezi Jumapili kabla ya mtanange siku ya kilele.

Mchezo dhidi ya St. George utakuwa kipimo kizuri kwetu baada ya mazoezi ya wiki tatu nchini Misri na itatupa dira kuelekea msimu mpya wa ligi 2022/23.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo tutawatambulisha wachezaji wetu tutakaowatumia msimu huu pamoja na benchi la ufundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER