Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa New Suez Canal kuikabili Al-Adalah inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Saudia Arabia katika mchezo wa kirafiki.
Mchezo dhidi ya Al-Adalah ni wa mwisho wa kirafiki hapa Misri na Julai 31 kikosi kitaanza safari ya kurejea nchini.
Jana tumecheza mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Telecom na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kocha Fadlu Davids anaendelea kutengeneza muunganiko wa wachezaji ndani ya timu hasa ukilinganisha wengi wao ni wageni ndani ya timu.