Tuna jambo letu kwa Mkapa leo

Kikosi chetu kitashuka leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao utaanza saa moja usiku.

Katika mchezo wa leo tunahitaji alama tatu muhimu ili kuendelea kupunguza tofauti ya alama kati yetu na wanaongoza.

Mchezo wa leo tunafahamu utakuwa mgumu, Mbeya Kwanza ni timu nzuri na itaingia uwanjani kuhakikisha inafanya vizuri ili kujiweka kwenye nafasi nzuri lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

KAULI YA MATOLA

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema tunatarajia kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Mbeya Kwanza na tutaipa heshima kubwa ili kutimiza lengo letu la kupata alama.

Matola ameongeza kuwa benchi la ufundi limeendelea kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza katika idara yetu ya ushambuliaji na anategemea kuanzia leo mabadiliko yataonekana.

“Mechi haiwezi kuwa rahisi na tunalijua hilo. Mbeya Kwanza ni timu nzuri tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kubaki na alama zote tatu.

“Tunajua suala la ukame wa mabao lipo kikosini, benchi la ufundi tumelifanyia kazi mazoezini na tunategemea kuanzia mchezo wa leo mabadiliko yataanza kuonekana,” amesema Matola.

KANOUTE AREJEA

Kiungo mkabaji, Sadio Kanoute ambaye alikosa mechi mbili zilizopita amerejea kikosini na amefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa leo baada yakuwa fiti.

Kanoute alipata maumivu kidogo ya mguu na alikosa mchezo wa hatua ya 32 ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Dar City pamoja na mechi ya Ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER