Tumezipata Pointi za Singida Fountain Gate

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate uliopigwa Uwanja wa Azam Complex umemalizika kwa kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya tano baada shuti la Clatous Chama kuokolewa na mlinda mlango Benedict Haule kabla ya kumkuta mfungaji.

Ntibazonkiza alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya tisa baada ya mlinzi Laurian Makame kuunawa mpira wa krosi uliopigwa na Israel Patrick.

Freddy Michael Kouablan alitupatia bao la tatu dakika ya 33 baada ya kumpoka Azizi Andambwile na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango.

Thomas Ulimwengu aliwapatia Singida bao la kwanza dakika ya 83 baada ya kumalizia pasi ya kichwa iliyopigwa na Yahaya Laurian Makame kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Amos Kadikilo.

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock (Kennedy 45′), Mzamiru (Kapombe 61′), Kibu (Onana 76′), Ngoma, Freddy (Jobe 76′), Ntibazonkiza, Chama

Walioonyeshwa kadi.

X1: Haule, Gyan, Mbegu, Makame, Carno, Andambwile (Kadikilo 51′), Kagoma, Kaseke (Kazadi 71′), Atta (Ulimwengu 71′), Ambundo (Wadada 51′), Kyombo (Hashim 81′)

Walioonyeshwa kadi: Andambwile 22′ Makame 88′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER