Tumezipata pointi tatu za Vipers

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Vipers katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo huo tulianza kwa kasi na kutafuta bao la mapema huku Vipers nao wakifanya mashambulizi ya haraka kila tunapopoteza mpira.

Dakika ya 41 tulifanya shambulizi la nguvu langoni mwa Vipers ambapo shuti kali lililopigwa na Saido Ntibazonkiza lilipanguliwa na mlinda mlango Alfred Mudekereza.

Clatous Chama alitupatia bao hilo pekee dakika ya 46 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Moses Phiri na kumlamba chenga mlinzi mmoja wa Vipers na kupiga shuti la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango Mudekereza.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi sita tukipanda hadi nafasi ya pili kwenye kundi C nyuma ya Raja Casablanca wenye alama 12.

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Henock, Kanoute, Chama, Mzamiru, Phiri (Baleke 74′), Ntibazonkiza (Erasto 90+3) Sakho (Banda 60′)

Walionyeshwa kadi: Phiri 70′

X1: Mudekereza, Mulondoo, Mubiru, Mandela, Mukundane, Osomba (Yiga 71), Sentamu (Lawal 86′), Watambala, Orit (Tety 54′) Lumala (Kizza 71′) Yunus.

Walionyeshwa kadi: Sentamu 70′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER