Tumezipata Pointi tatu za Singida

Kikosi kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Liti.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukilifikia zaidi lango la Singida na kutengeneza nafasi ingawa hatukizitumia vizuri.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya 26 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Kibu Denis.

Kipindi cha pili Singida walirudi kwa kasi na kuongeza mashambulizi langoni kwetu lakini tulikuwa imara kuhakikisha hatuwapi nafasi.

Singida walisawazisha bao hilo dakika ya 51 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elvis Rupia.

Moses Phiri alitupatia bao la pili dakika ya 83 baada ya kupokea pasi ya Luis Miquissone ambaye alipokea krosi ya Shomari Kapombe.

Ushindi huu unatufanya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 15 tukiwa hatujapoteza wala kupata sare yoyote.

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Ngoma, Chama (Miquissone 57′), Mzamiru (Kanoute 57′), Bocco (Phiri 45′), Ntibazonkiza (Baleke 66′), Kibu (Israel 86′)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Kakolanya, Gyan (Wadada 64′), Gadiel, Waziri (Makame 81′), Carno, Kagoma, Andambwile, Abuya, Bruno (Kaseke 45′), Tchakei, Rupia

Walioonyeshwa kadi: Kakolanya 22′ Andambwile 54′ Hamadi 79′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER