Tumezipata pointi tatu za Ruvu Shooting

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikifika langoni kwa mpinzani lakini nafasi zilizotengenezwa hazikutumiwa vizuri.

Clatous Chama alitupatia bao la kwanza dakika ya 30 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kufika zaidi langoni mwa Ruvu Shooting lakini hata hivyo mashambulizi tuliyofanya yaliishia mikononi mwa mlinda mlango, Abdallah Rashid.

Pape Sakho alitupatia bao la pili dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Saido Ntibazonkiza aliyotoka na mpira katikati ya uwanja.

Sakho alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tatu dakika ya mwisho ya mchezo akimalizia tena krosi ya Ntibazonkiza.

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Kennedy, Mkude, Chama (Banda 87′), Mzamiru, Baleke (Sakho 59′), Ntibazonkiza, Kibu (Bocco 87′)

Walioonyeshwa kadi: Mkude 69′

X1: Rashid, Maicon (Kaberege 77), Mwakinyuke, Mtui, Msonjo, Dabi, Chonongo, Msala, Kassim, Mashaka, Patrick (Onesmo)

Walioonyeshwa kadi: Msonjo 68′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER