Tumezipata pointi tatu za Mashujaa Chamazi

Kikosi chetu kimefanikiwa kupata pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukiliandama lango la Mashujaa huku tukitengeneza nafasi lakini hatukuwa makini kwenye kuzitumia na kusababisha mchezo kwenda mapumziko

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo Clatous Chama akitupatia la kwanza dakika ya 56 baada ya kumalizia pasi ya Willy Onana.

Chama akitupia bao la pili dakika ya 73 baada ya kumalizia mpira wa krosi ukiopigwa na Zimbwe Jr.

Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Mashujaa na kuzidi kutengeneza nafasi lakini hatukuweza kuzitumia vizuri huku Mashujaa wakionekana kurudi wote nyuma.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock (Kennedy 80′), Babacar (Mzamiru 74′), Kibu (Miqussone 74′), Ngoma, Freddy (Onana), Ntibazonkiza, Chama (Jobe 88:)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Munthary, Kindamba, Mwakinyuke, Madeleke, Ame, Masinda, Omary (Balama), Stambuli, Jeremanus, Ulomi, Adam (Assa 77′)

Walioonyeshwa kadi: Michael Masinda 22′ Madeleke 51′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER