Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi umemalizika kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Geita walipata bao la kwanza kupitia kwa Jofrey Julius dakika ya 11 baada ya mlinda mlango Hussein Abel kukosea kucheza mpira wa krosi uliopigwa na Edmund John.
Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia lango la Geita na kutengeneza nafasi lakini tulikosa umakini katika eneo la mwisho.
Saido Ntibazonkiza alitusawazishia bao hilo dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Geita walimaliza mechi wakiwa pungufu kufuatia nahodha Michael Onditi kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 68 baada ya kumfanyia madhambi Willy Onana.
Ntibazonkiza alitupatia bao la pili dakika ya 71 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya Onana kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Ladaki Chasambi alitupatia bao la tatu dakika ya 85 baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Willy Onana.
Chasambi alipigilia msumari wa nne dakika ya 93 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.
X1:Abel, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Ngoma (Karabaka 80′), Balua (Onana 65′) , Mzamiru, Jobe (Kanoute 65′), Ntibazonkiza, Chasambi
Walioonyeshwa kadi:
X1: Costa Jr, Maganga, Mlingo, Kyaruzi, Mahamud, Onditi, Dunia, Julius (Ulaya 45′), Edmund, Kiakala (Mashaka 72:), Saadun
Walioonyeshwa kadi: Tariq Seif 56′ Onditi 56, 68 Yusuph Dunia 75′