Tumezindua Simba Executive Networks Dodoma

Klabu yetu ikishirikiana na Benki ya NMB imezindua Simba Executive Networks jijini Dodoma kwa ajili ya kukusanya mapato ambapo Naibu Spika wa Bunge, Azan Zungu alikuwa Mgeni rasmi.

Mara ya kwanza mradi kama huu ulizinduliwa jijini Dar es Salaam, Machi mwaka huu na leo umefanyika Dodoma ili kukusanya mapato.

Mtendaji Mkuu wa Klabu Imani Kajula amesema ili uwe mwanachama wa Simba Executive Networks unatakiwa kulipia Shilingi 1,500,000 kwa mwaka ambapo utapewa kadi Maalum ambayo itamuwezesha kupata mambo mbalimbali kama nafuu kwenye Maduka makubwa Viwanja vya Ndege.

Vitu vingine ni kupata punguzo kwenye manunuzi ya tiketi katika mechi zetu mbalimbali hasa za zile kubwa za Kimataifa.

CEO Kajula amesema jambo la kwanza ambalo pesa hizo zitafanya ni kukarabati Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kwa kuweka taa pamoja na majukwaa ili timu za Vijana na Wanawake waweze kucheza mechi zao za mashindano.

Mgeni rasmi Mh. Zungu ameusisitiza Uongozi kutumia wingi wa wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram kuongeza mapato ambayo yatakuwa msaada kwa Klabu.

Mh. Zungu ameongeza kuwa kwa sasa ndio wakati wakuwa kitu kimoja na kuondoa makundi ili kuirudisha timu katika ubora wake.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER