Ikiwa imepita siku moja tangu Kibegi kilichobeba jezi za msimu 2023/24 na kwenda kuzinduliwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kupigwa mnada na kuuzwa kwa Sh. 2,500,000 leo tumezindua ‘Kibegi Part Two’ katika Uzinduzi wa hamasa ya Wiki ya Simba uliofanyika Buza Kanisani.
Ndani ya Kibegi part Two kuna kitu kinaitwa shabiki bingwa ambapo mashabiki 20 watapatiwa tiketi ya Platinum ya kuingilia Simba Day, Agosti 6 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Shabiki bingwa kutoka Kibegi Part Two usafiri utamfuata popote alipo hadi hotelini na baadae anapelekwa uwanjani na baada ya mechi atarudishwa hadi nyumbani kwakwe.
Kwa wale wanaotokea mikoani watawalipiwa tiketi ya Ndege na watapokelewa Airport na kupelekwa hotelini na baadae uwanjani, mechi ikiisha anakatiwa tiketi ya kurudi alipotoka.
Ilikupata tiketi ya shabiki bingwa unatakiwa kuwa ni Shilingi 1000 pekee.
Unaweza kushiriki shabiki bingwa kupitia mtandao wowote wa simu ulionao.
Utaratibu upo hivi.
🔸Nenda kwenye LIPA BILI
🔸Ingiza namba ya Kampuni 909192
🔸 Kumbukumbu namba andika neno SIMBA
🔸Kiasi weka Sh. 1000
🔸 Ingiza namba ya siri.
Shiriki mara nyingi ili kujiweka kwenye mazingira ya kupata nafasi ya kuwa shabiki bora.
Zoezi la shabiki bora litaendelea hata baada ya Simba Day, tutalitumia pia kwenye michezo ya Ngao ya Jamii pamoja na michuano ya kimataifa.