Tumezindua Chaneli ya Whatsapp

Klabu yetu imekuwa ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuzindua Chaneli yake ya Whatsapp kwa ajili ya kuwasiliana na mashabiki wetu moja kwa moja.

Katika kipindi hiki cha mapinduzi makubwa ya kidigitali Whatsapp ndio Chaneli iliyopakuliwa zaidi duniani kuliko yoyote.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema Whatsapp wenyewe wamekuja kwetu na kutaka ushirikiano nasi kutokana na wingi wa mashabiki tulionao.

CEO Kajula amesema Chaneli ya Whatsapp itatuwezesha kutoa taarifa na kuwafikia mashabiki wetu kwa haraka kupitia kwenye magroup ambapo pia tutaweza kuwatangaza wadhamini wetu.

“Mara zote Simba ndio waanzilishi wa kila kitu. Tunaongoza kuwa na wafuasi wengi Instagram, Facebook Youtube sasa tunahamia Whatsapp lengo ni moja tu kwenda sawa na dunia ya kidigitali inavyotaka.

“Whatsapp Chaneli inazidi kushika chati duniani klabu kama Manchester United, Barcelona na Real Madrid ni miongoni mwa zinazotumia wakati Orlando Pirates na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini nazo pia zimo kwahiyo nasi Simba hatutaki kupitwa na masuala ya kiteknolojia,” amesema CEO Kajula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER