Tumewashika mkono Mahabusu ya Watoto Upanga

Klabu yetu kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation, leo tumetembelea Mahabusu ya Watoto Upanga na kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Shughuli za Kijamii kuelekea maadhimisho ya Simba Day ambayo kilele chake itakuwa Agosti 8, mwaka huu.

Kama ada yetu tumetoa misaada mbalimbali kama unga, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za unga, sabuni za mche, maji ya kunywa na juisi.

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema kila mwaka tunatoa misaada lakini safari tumejitahidi kuwafikia wale ambao si rahisi kufikiwa kama hapa kwenye mahabusu ya watoto.

“Tangu Julai 31 tulivyoanza shughuli za kijamii tumekuwa tukiwafikia wenye uhitaji ambao imekuwa ngumu kukumbukwa kama tulivyofanya kwenye kambi ya wazee ya Nungu ya Kigamboni na leo hapa Upanga,” amesema Ahmed.

Kwa upande wake Meneja wa Kituo, Darius Kalijongo ameshukuru upendo tulioonyesha na misaada tuliyowapa ambayo amekiri itawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku.

“Tunawashukuru Simba kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation kwa msaada huu, mmeonyesha upendo mkubwa, pia tunawaomba taasisi nyingine kufanya kama Simba kwa kuwa hawa watoto wanahitaji faraja na upendo kama watu wengine,” amesema Kalijongo.

Mahabusu ya Upanga inaweza kuwahudumia watoto 60 lakini kwa sasa kina watoto 14 wavulana 12 na wasichana wawili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER