Tumewashika mkono Kituo cha Wazee Kigamboni

Klabu yetu kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation leo tumetoa misaada mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee cha Nunge kilichopo Kigamboni ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii kuelekea Tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 8.

Misaada hiyo ni unga wa ngano, mafuta ya kupikia, sukari na sabuni ya unga, sabuni za mche ambazo zitasaidia katika maisha yao kila siku.

Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amesema leo Tanzania nzima inafanya shughuli za kijamii uongozi umekuja hapa kwa kuwa wazee ni kundi ambalo limesahulika.

“Ni jukumu letu kuwalea wazee wetu kwa kuwa hawana mtu wa kuwaangalia na kuwapa upendo, Simba na Mo Dewji Foundation tumeona tuwafikie tuwape sadaka zetu kikubwa tunaomba mtuombee ili tutimize malengo yetu ya kurudisha mataji msimu ujao,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Makazi ya wazee Nunge, Jacklina Kanyamwenge ameishukuru klabu na Mo Dewji Foundation kwa sadaka hii ambapo amesema ni msaada mkubwa huku akiziomba taasisi nyingine kuwa na moyo wa kutoa kwa watu wenye uhitaji kama tulivyofanya sisi.

“Kambi yetu ina wazee 22 wanaume wakiwa 12 na wanawake 10. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1936 kwa ajili ya wenye ugonjwa wa ukoma lakini sasa wazee wenye ulemavu wa aina yoyote wapo hapa tunawalea,”

“Simba na Mo Dewji Foundation mmefanya jambo kubwa ambalo limegusa maisha ya watu wengi ambao hawana msaada na hili linasisitizwa hadi kwenye vitabu vya dini,” amesema Kanyamwenge.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER