Tumewapa zawadi ya Mwaka Mpya mashabiki wetu

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao tunautoa kwa mashabiki kama sehemu ya zawadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya.

Tulianza mchezo huo kwa kasi na kuliandama lango la Azam ambao walianza taratibu wakizuia muda mrefu na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Rally Bwalya alikosa mkwaju wa penati dakika ya 15 baada ya Pape Sakho kufanyiwa madhambi na walinzi wa Azam ndani ya 18.

Baada ya tukio hilo tuliendelea kuliandama lango la Azam tukicheza zaidi upande wao lakini tulikosa umakini wa kumalizia nafasi tulizotengeneza.

Sadio Kanoute alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 68 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na mlinzi Mohamed Hussein.

Sakho ambaye ameonyesha kiwango safi katika mchezo wa leo alitufungia bao la pili dakika ya 72 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Kanoute.

Azam walipata bao lao kupitia kwa mshambuliaji Rogers Kola aliyeweka mpira kifuani na kupiga shuti lililotinga wavuni moja kwa moja.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Medie Kagere, Bwalya Sakho na Kibu Denis na kuwaingiza Chris Mugalu, Hassan Dilunga Mzamiru Yassin na Pascal Wawa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER