Tumewapa furaha tuliyowaahidi Wanasimba

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya St.George ya Ethiopia kwenye kilele cha Simba Day mtanange uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kibu Denis alitupatia bao la kwanza dakika ya 19 kwa shuti kali ndani ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa St. George baada ya shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.

Baada ya bao hilo St.George waliongeza mashambulizi langoni kwetu ambapo dakika ya 23 almanusura wasawazishe lakini mpira wa kichwa uliopigwa na kiungo wao ulitoka nje kidogo ya lango.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER