Tumevuna pointi tatu za Dodoma Jiji

 

Kikosi chetu kimefanikiwa kupata pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tulianza mchezo kwa umiliki mkubwa dakika ya nne tulipata bao la kwanza baada ya mlinzi wa Dodoma Jiji Abdallah Shaibu kujifunga katika jitihada za kuokoa mpira uliopigwa na Clatous Chama.

Moses Phiri alitupatia bao la pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 dakika ya 44 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jonas Mkude.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo dakika 20 za kwanza tulitengeza nafasi nyingi ambazo hata hivyo hatukizitumia vizuri.

Habib Kyombo alitupatia bao la tatu kwa kichwa cha chini chini dakika ya 84 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa John Bocco, Kibu Denis na Phiri na kuwaingiza Kyombo, Nelson Okwa na Erasto Nyoni.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 13 na kurejea kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi tano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER