Tumetolewa Shirikisho Afrika kwa penati

Timu yetu imetolewa kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mikwaju ya 4-3 ugenini dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Tulienda katika hatua ya mikwaju ya penati kutokana na sare ya kupoteza kwa bao moja ikifanya kuwa sare kufuatia ushindi kama huo tuliopata nyumbani.

Mchezo ulianza kwa kasi huku wenyeji Orlando wakionyesha kuhitaji kupata bao la mapema lakini kikosi chetu kilionyesha utulivu mkubwa.

Tulifanya mashambulizi machache ya kushtukiza tukipitia zaidi upande wa kulia alipokuwa Shomari Kapombe na Israel Patrick ingawa krosi zao hazikuwa na madhara makubwa kwa Orlando.

Dakika ya 57 mshambuliaji Chris Mugalu alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada kumkanyaga mlinzi wa kati wa Orlando.

Kwame Peprah aliwapatia Orlando bao la kwanza dakika ya 59 kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kushoto.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Israel Patrick na Pape Sakho na kuwaingiza Taddeo Lwanga na Medie Kagere.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER