Kikosi chetu kimeshindwa kutinga fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kupoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Polisi Bullets kutoka Kenya.
Mchezo huo ulikuwa mkali muda wote huku timu zikishambuliana kwa zamu huku zikitaka kupata bao la mapema ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.
Polisi walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 30 baada ya Lucy Jira kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Caroline Rufa.
Vivian Corazone alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 39 baada ya kutumia vizuri makosa ya mlinda mlango wa Polisi Kwasi.
Vivian alitupatia bao la pili dakika ya 56 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Elizabeth Wambui.
Dakika ya 63 Diana Mwihaki aliisawazishia Polisi kwa kichwa mpira wa adhabu ulopigwa na Lydia Akoth.
Dakika ya 82 Rebecca Okwaro aliwapatia Polisi bao la tatu dakika ya 82 na kuwapeleka fainali.
Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Preicous Christopher, Ritticia Nabbosa na Violeth Nicholas na kuwaingiza Asha Djafar, Asha Mwalala na Esther Mayala.
Matokeo haya yanatufanya kukutana na mshindi kati ya Kawempe Muslim na CBE katika mchezo wa kumtamfuta mshindi wa tatu.