Mchezo wetu wa nusu fainali ya Azam Sports Federation dhidi ya Azam FC umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-1 katika mtanange uliopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza dakika ya 22 kupitia kwa Lusajo Mwaikenda baada ya mlinda mlango Ally Salim kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na Ayoub Lyanga kabla ya kumkuta mlinzi huyo wa kulia.
Sadio Kanoute alitupatia bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya 27 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Saido Ntibazonkiza.
Prince Dube aliwapatia Azam bao la pili dakika ya 75 muda mfupi baada ya kutoka benchi akimalizia pasi ya kichwa ya Lyanga.
Kanoute alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 87 kufuatia kumchezea vibaya James Akaminko.
X1: Idrisu, Mwaikenda, Kangwa, Kheri, Ndala, Lyanga (Chilambo 90+3), Bajana, Mbombo (Dube 69′) Akaminko, Sopu.
Walioonyeshwa kadi: Bajana 19′
X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Henock, Kanoute, Chama, Mzamiru, Baleke (Bocco 81′) Ntibazonkiza, Kibu (Sakho 82′)
Walioonyeshwa kadi: Kanoute 70′ 86′ Inonga 90+1