Tumetolewa michuano ya U20

Kikosi chetu cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kimetolewa kwenye michuano ya vijana baada kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam katika mchezo wa mwisho wa makundi uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku Azam wakimiliki zaidi na kucheza kwa kasi wakionekana kutafuta bao la mapema.

Wenyeji wa mchezo Azam ambao walikuwa bora muda mwingi walipata bao la kwanza dakika ya 24.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi kutaka kutafuta bao la kusawazisha lakini nyota wetu walikosa umakini wa kutumia nafasi tulizotengeneza.

Cyprian Kachwele aliwapatia Azam bao la pili dakika ya 78 akimlaizia mpira uliorudi baada ya kugonga mwamba akiwa ndani ya 18.

Matokeo haya yametufanya kutolewa kwenye michuano hii tukiwa tumepata alama moja pekee tukifungwa mechi mbili na kutoka sare moja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER