Tumetolewa Ligi ya Mabingwa Afrika

Mchezo wetu wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliopigwa Uwanja wa Cairo International umemaliza kwa kupoteza kwa mabao 2-0.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukishambulia lango la Al Ahly lakini tulipoteza nafasi kadhaa tulizotengeneza.

Amr El Soulia aliwapatia wenyeji Al Ahly bao la kwanza dakika ya 47 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Anthony Modeste.

Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya kutafuta bao la kusawazisha na kuongeza nyingine lakini wenyeji Al Ahly walikuwa imara zaidi.

Al Ahly walipata bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo kupitia kwa Mahmoud Kahraba baada ya mlinzi Che Malone kumchezea madhambi Hussein El Shahat ndani ya 18.

X1: Shobeir, Abd ElMonem, Rabia Hany, Maaloul (Eldebes 90+5′) Marawan, Koka, El Soulia (Moursy 85′), El Shahat, Reda Slim (Taher 85′), Modeste (Abdelhamid 85′).

Walioonyeshwa kadi:

X1: Lakred, Kapombe (Israel 74′) Zimbwe Jr Che Malone Henock Ngoma, Ntibazonkiza (Jobe 82′), Babacar, Kibu (Onana 82′), Kanoute (Miqussone 74′), Chama (Freddy 89′)

Walioonyeshwa kadi: Kibu 65′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER