Tumetolewa kwa mikwaju ya penati Morocco

Safari yetu ya Ligi ya Mabingwa imefikia tamati baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penati 4-3 na Wydad Casablanca katika mchezo wa marudiano uliopigwa uwanja wa Mohamed wa V nchini Morocco.

Katika dakika 90 za kawaida tulifungwa bao moja kama ambavyo tuliwafunga Wydad nyumbani katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikisomana na kusababisha mpira kuchezwa zaidi katikati ya uwanja na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Wenyeji Wydad walipata bao lao dakika ya 24 kwa kichwa kupitia kwa Bouly Sambou baada ya walinzi kuzembea kuruka juu pamoja na mfungaji.

Penati zetu tatu zilifungwa na Erasto Nyoni, Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri wakati Shomari Kapombe na Clatous Chama wakipoteza.

X1: El Motie, Benayada (El Nabi 83′), Aboulfath, Jabrane, Daoudi (Haimoud 68), El Hassouni, Attiat Allah, Sambou, Boussefian (Ounnajem 68), Bouhra (Moutaraji), Kiaku.

Walioonyeshwa kadi: El Moutaraji 90+2′

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Henock, Kanoute, Chama, Mzamiru, Baleke (Erasto 84′), Ntibazonkiza, Kibu (Phiri 90+5)

Walioonyeshwa kadi: Chama 7′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER