Tumetolewa ASFC

Mchezo wetu wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Feisal Salum aliwapatia Yanga bao hilo pekee dakika ya 25 kwa shuti kali alilopiga nje ya 18 na kumshinda mlinda mlango Beno Kakolanya.

Kipindi cha pili Kocha Pablo Franco alimuingiza Rally Bwalya kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika eneo la mwisho la ushambuliaji akichukua nafasi ya Taddeo Lwanga.

Kibu Denis alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia sehemu ya juu kidogo na jicho iliyosababisha
kufungwa bendeji na nafasi yake ikachukuliwa na Yusuf Mhilu huku akiingia Medie Kagere kumpokea Mzamiru Yassin.

Jimmyson Mwanuke naye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumizwa na Fiston Mayele nafasi yake ikachukuliwa na Erasto Nyoni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER