Tumetoka sare na Azam Kirumba

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Prince Dube aliwapatia Azam bao la kwanza dakika ya 14 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Pascal Msindo.

Baada ya bao hilo tulifanya jitihada za kutaka kusawazisha lakini hata hivyo tulikosa umakini wa kutumia nafasi.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi katika kutaka kusawazisha lakini Azam walikuwa nyuma muda mwingi.

Clatous Chama alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 92 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya Pa Omar Jobe kufanyiwa madhambi nje ya 18.

X1: Ayoub, Israel (Kapombe 45′), Zimbwe Jr, Che Malone, Kazi (Kennedy 45′), Sarr, Kibu, Ngoma (Mzamiru 71′), Fred (Jobe 45′), Ntibazonkiza (Miqussone 75′), Chama

Walioonyeshwa kadi: Kazi 45′ Chama 58′ Jobe 90+4′

X1: Mustafa, Lusajo, Msindo (Sidibe 74′), Bangala (Amoah 45′), Fuentes, Akaminko, Bin Zayd, Syllah, Dube (Navarro 79′), Fei Toto (Lyanga 79′), Sopu.

Walioonyeshwa kadi: Syllah (37′) Amoah 90′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER