Tumetoka sare na Al Hilal kwa Mkapa

Mchezo wetu wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Makabi Lilepo aliwapatia Al Hilal bao la mapema dakika ya sita baada kumalizia pasi ya mpira wa adhabu iliyopigwa na mlinzi wa kushoto Ibrahima Emora.

Winga Augustine Okrah alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata maumivu ya msuli na kutolewa dakika ya 15 nafasi yake ikachukuliwa na Habib Kyombo.

Mshambuliaji Jean Baleke nae alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 33 baada ya kupata maumivu nafasi yake ikachukuliwa na nahodha John Bocco.

Kipindi cha pili kocha Robertinho alifanya mabadiliko kuwaingiza Clatous Chama, Pape Sakho, Mohamed Hussein Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Nassor Kapama na Mohamed Mussa kuchukua nafasi za Gadiel Michael, Peter Banda, Kibu Denis na Jimmyson Mwanuke, Erasto Nyoni, Ismael Sawadogo na Sakho

Baada ya mabadiliko hayo tuliongeza kasi katika eneo la kushambulia ambapo Kyombo alitusawazishia bao hilo dakika ya 81 kwa shuti kali ndani ya 18 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Sakho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER