Tumetinga Robo Fainali ASFC

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuifunga African Sports katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya 36 akimalizia mpira mrefu kutoka katikati ya uwanja uliopigwa na Pape Sakho.

Mlinzi wa kati, Kennedy Juma alitupatia bao la pili dakika ya 47 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Moses Phiri.

Mohamed Mussa alitupatia bao la tatu dakika ya 69 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Phiri.

Jimmyson Mwanuke alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia bao la nne dakika ya 89 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Peter Banda.

Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alifanya mabadiliko ya kuwatoa Sakho, Habib Kyombo, Phiri, Erasto Nyoni na kuwaingiza Peter Banda, Mohamed Mussa, Mwanuke, Clatous Chama na Nassor Kapama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER