Tumetinga Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Jamhuri bao moja katika mchezo uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Tulianza kwa kasi huku tukilifikia zaidi lango la Jamhuri lakini walikuwa imara ambapo mashambulizi yetu mengi yaliishia kwa walinzi wao.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 46 kipindi cha kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Luis Miqussone.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kufanya mashambulizi mengi lakini ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata ulikuwa mdogo.

Matokeo yanatufanya kukutana na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Nusu Fainali utakaopigwa Jumatano Januari 10.

X1: Lakred, Kapombe, Israel, Kennedy, Che Malone, Ngoma, Miqussone (Karabaka 69′), Abdallah (Chilunda 46′) (Mussa 90+1), Baleke (Phiri 69′), Ntibazonkiza (Sarr 69′), Onana

Wachezaji wa Akiba: Baleke 55′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER