Tumetinga Nusu Fainali Shirikisho Afrika Kibabe

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga Al Masry kwa mikwaju ya penati 4-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo ulienda kwenye mikwaju ya penati kufuatia ushindi wa mabao 2-0 tuliopata kwenye dakika 90 za kawaida matokeo ambayo yalitokea katika mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Misri.

Elie Mpanzu alitupatia bao la kwanza dakika ya 22 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea mpira wa kurusha kutoka kwa Shomari Kapombe.

Steve Mukwala alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 32 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Kipindi cha pili Al Masry walitumia muda mwingi kupoteza muda huku tukifanya mashambulizi mengi langoni kwao lakini walikuwa imara kwenye kujilinda.

Penati zetu zilifungwa na Jean Charles Ahoua, Steven Mukwala, Kibu Denis na Shomari Kapombe.

X1: Camara, Kapombe Zimbwe Jr (Nouma 75′) Chamou, Hamza, Kagoma Kibu Ngoma (Awesu 89′), Mukwala, Ahoua, Mpanzu

Walioonyeshwa kadi:

X1: Mahmoud, Moursi, Youssef, Makhlouf, Salah, Amr, Mahmoud, Ahmed, Samadou, Khaled (Ben Yussif 89′), Deghmoum (Bambo 90+5)

Walioonyeshwa kadi: Eid 50′, Makhlouf 56′ Mido 79′ Gad 83′ El Mohamady 88′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER