Tumetinga Nusu Fainali Mapinduzi Cup

Ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Selem View uliopigwa Uwanja wa Amani umetufanya kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar.

Licha ya ushindi wa mechi moja tumetinga nusu fainali kutokana na kundi letu kuwa na timu tatu hivyo tumesalia na mchezo mmoja ambao tutacheza Ijumaa.

Pape Sakho alitupatia upbao la kwanza dakika ya 25 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Gadiel Michael kutoka upande wa kushoto.

Rally Bwalya alitupatia bao la pili dakika ya 53 kwa shuti kali lililotinga wavuni moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango wa Selem.

Kocha Pablo Franco aliwaingiza Chris Mugalu, Yussuf Mhilu Check Tenena, Israel Patrick na Sharaf Eldin Shiboub na kuwatoa Pape Sakho, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute na Jimmyson Mwinuke.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER