Tumetinga Nusu Fainali CECAFA

Ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Kawempe Muslim kutoka Uganda umetuwezesha kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Katika mchezo huo ulikuwa mkali muda wote timu zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana kutokana na ubora waliokuwa nao Kawempe uliochangiwa na hali ya hewa ya baridi kali kwa wachezaji wetu.

Vivian Corazone alitupatia bao la kwanza dakika ya 64 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Precious Christopher.

Dakika tano baadae Jentrix Shikangwa alitupatia bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Precious.

Elizabeth Wambui alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 75 kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Kawempe Adeke Juliet.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Amina Bilali, Ritticia Nabbosa, Jackline Albert, Daniela Ngoyi na Saiki Mary na kuwatoa Asha Rashid, Asha Djafari, Precious, Vivian na Wincate Kaari.

Ushindi huu umetupa tiketi ya moja kwa moja ya nusu fainali ambapo mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya PVP Buyenzi ya Burundi utakaopigwa Agosti 23 utakuwa wa kukamilisha ratiba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER