Tumetinga Nusu Fainali ASFC

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuifunga Pamba FC mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo katika dakika 10 za mwanzo tulikuwa tumefika langoni mara tano ambapo tulipoteza nafasi za wazi za kufunga.

Baada ya kosa kosa nyingi Peter Banda alitupatia bao la kwanza dakika ya 44 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Rally Bwalya.

Dakika ya 47 Kibu Denis alitupatia bao la pili kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Yusuf Mhilu alitupatia bao la tatu kwa kichwa dakika ya 52 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Jimmyson Mwanuke kutoka upande wa kulia.

Muhilu alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne dakika ya 88 baada ya kumalizia krosi iliyopigwa na Gadiel Michael.

Kocha Pablo Franco aliwatoa John Bocco, Kibu, Zimbwe Jr, Bwalya na Mzamiru Yassin na kuwaingiza Medie Kagere, Pape Sakho, Sadio Kanoute, Gadiel na Taddeo Lwanga.

Ushindi huu unatufanya kukutana na watani wetu wa jadi Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ambapo utapigwa mwezi ujao.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER