Tumetinga hatua ya makundi Shirikisho kibabe

Tumefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Ahli Tripoli mtanange uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Cristovao Mabulu aliipatia Al Ahli Tripoli bao la kwanza dakika ya 17 kufuatia mlinzi wa kati Che Fondoh Malone kurudisha mpira wa kichwa ambao ulikuwa mfupi kwa mlinda mlango Moussa Camara kabla ya kumkuta mfungaji.

Kibu Denis alitupatia bao la kusawazisha dakika 36 kwa mpira wa tiktak ya mguu wa kushoto baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Che Malone.

Leonel Ateba alitupatia bao la pili dakika ya 46 baada ya mlinzi wa kati Murad Hedhili kukosea kutoa pasi kabla ya kumkuta mfungaji.

Edwin Balua alitupatia bao la tatu dakika ya 90 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka nyuma kabisa.

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Hamza (Karaboue 45′), Kagoma (Ngoma 75′) Kibu (Okajepha 75′), Fernandes, Ateba, Ahoua (Kijili 85′), Mutale (Balua 81′)

Walioonyeshwa kadi: Ateba 60′

X1: Altihar, Thierry, Masaud, Eltrbi, Abdu Salam, Chaleli (Akrawa 64′), Hedhili, Tayfour, Bisharah (Mohamed 64′), Paciencia, El Houni

Walioonyeshwa kadi: Sand Masaud 17′ El Houni 37′ Thierry Manzi

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER