Tumetinga hatua ya 16 ASFC kwa kishindo

Kikosi chetu kimetinga hatua ya 16 bora ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya TRA kutoka Kilimanjaro katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute amefunga mabao matatu peke yake hat trick katika mchezo huo huku akifunga moja kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili.

Ladaki Chasambi alitupatia bao la kwanza dakika ya 13 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia kazi iliyofanywa na Freddy Michael.

Sadio Kanoute alitupatia bao la pili dakika ya 40 kwa shuti la chini chini ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi safi ya mpira adhabu iliyopigwa na Mzamiru Yassin.

Freddy Michael alitupatia bao la tatu dakika ya 52 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Chasambi.

Kanoute aliongeza bao la nne na latano dakika ya 54 na 56 akimalizia pasi za Kibu Denis na Mzamiru.

Pa Omar Jobe alitupatia bao la sita dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Edwin Balua.

Ushindi huu unatufanya kukutana na Mashujaa FC katika mchezo wa hatua inayofuata ya 16 bora.

X1: Manula, Duchu, Israel, Kennedy, Kazi, Kanoute, Hamis (Balua 68′), Mzamiru (Babacar 76′), Freddy (Jobe 68′), Chasambi ( Karabaka 68′), Kibu (Miqussone 68′)

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER