Tumetinga Fainali ya michuano ya Muungano

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Muungano baada ya kuifunga KVZ mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Katika mchezo huo tulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la KVZ na kutengeneza nafasi.

Freddy Michael alitupatia bao la kwanza dakika ya 26 ya kuwazidi ujanja walinzi wa KVZ.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kufanya mashambulizi ili kupata mabao zaidi lakini KVZ walikuwa imara kwenye kuzuia.

Israel Patrick alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya nne ya nyongeza kipindi cha pili baada ya Pa Omar Jobe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kiungo mkabaji Fabrice Ngoma amechaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kukabidhiwa Shilingi 300,000 kutoka kwa wadhamini Bank ya PBZ.

Baada ya ushindi wa leo tunamsubiri mshindi kati ya Azam FC dhidi ya KMKM katika mchezo wa fainali.

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy Che Malone, Ngoma, Chasambi (Onana 62′), Mzamiru (Hamis 79′), Freddy (Jobe 62′), Chama (Miqussone 32′), Kibu (Karabaka 69′)

Walioonyeshwa kadi: Ngoma 90(3

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER