Tumetinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Singida Fountain Gate kwa mikwaju ya penati 3-2 kufuatia kutoka sare ya bao moja kwenye muda wa kawaida.

Elvis Rupia aliwapatia Singida bao la mapema dakika ya 11 baada ya mlinzi wetu Kennedy Juma alikosea kwa kumpa mpira Marouf Tchakei ambaye alitoa pasi kwa mfungaji.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kutafuta bao la kusawazisha lakini Singida walikuwa makini katika safu ya ulinzi kuhakikisha wanakuwa salama muda wote.

Fabrice Ngoma alitupatia bao la kusawazisha dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya mpira na kona uliopigwa na Saido Ntibazonkiza kuokolewa kabla ya kumkuta mfungaji akiwa ndani ya 18.

X1: Ally Salim, Kapombe, Israel Patrick, Che malone, Kennedy (Kazi 45:), Ngoma, Babacar (Miqussone 60′), Kanoute, Baleke (Phiri 45′), Ntibazonkiza, Onana (Karabaka 76′)

Walionyeshwa kadi

X1: Ibrahim, Kijili, Gadiel, Mangalo, Carno, Kagoma (Hamad 65′), Chukwu, Kaseke, Tchakei (Kadikilo 89′), Rupia (Kagere 72′), Abuya

Walioonyeshwa kadi: Gadiel 45′ Mangalo 51, Kaseke 89′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER