Tumetinga 32 bora ya ASFC

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuifunga Tembo FC kutoka Tabora mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex.

Luis Miqussone alitupatia bao la kwanza dakika ya 10 kwa shuti kali la chini chini ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Fred Michael.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 31 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Sadio Kanoute.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuliandama lango la Tembo lakini mlinda mlango wao alikuwa makini kuhakikisha wanakuwa salama.

Saleh Karabaka alitupatia bao la tatu dakika ya 81 baada ya kupokea pasi ya upendo kutoka kwa Ntibazonkiza.

Dakika moja baadae Pa Omar Jobe alitupatia bao la nne kwa shuti kali akiwa nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ntibazonkiza.

X1: Abel (Feruz 90′), Israel, Kennedy, Kazi, Kapombe, Miqussone (Chasambi 72′), Kanoute, Fred (Karabaka 72′), Ntibazonkiza, Balua (Jobe 45′)

Walioonyeshwa kadi: Kanoute 70′ Kapombe 75′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER