Ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umetufanya kuingia hatua ya 32 bora ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku JKT wakicheza zaidi nyuma na kutumia mipira mirefu ambayo hata hivyo haikuwa na madhara na kutuacha kutawala mechi.
Kibu Denis alitupatia bao la kwanza dakika ya 27 kwa shuti kali la mguu wa kulia akiwa ndani ya 18 kufuatia mpira mrefu uliopigwa na Pascal Wawa kuzuiwa na mlinzi wa kati JKT kabla ya kumkuta mfungaji.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi kutafuta bao la pili huku JKT wakiendelea kubaki nyuma na kumfanya mlinda mlango wetu Beno Kakolanya kuwa likizo muda mrefu.
Kocha Pablo Franco aliwatoa Kibu, Israel Patrick, Yusufu Mhilu, Pape Sakho na Peter Banda kuwaingiza Shomari Kapombe, Duncan Nyoni, Jimmyson Mwanuke, Ibrahim Ajibu na Medie Kagere.

One Response