Tumetinga 16 bora ASFC

 

Ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya Coastal Union umetuwezesha kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tulianza mchezo kwa kasi kwa kutengeneza nafasi na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini Coastal walikuwa imara katika safu yao ulinzi na tulishindwa kupenya.

Ilituchukua dakika 10 za kipindi cha pili kupata bao la ushindi kwa shuti kali la chini chini nje kidogo cha 18 kuptia kwa Sadio Kanoute baada ya kupokea pasi ya Pape Sakho.

Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia lango la Coastal huku ‘Wagosi hao’ wakicheza kwa makini katika safu ya ulinzi.

X1: Kakolanya, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Onyango, Sawadogo (Mzamiru 59′) Sakho (Kibu 59′) Kanoute, Baleke (Okrah 87′) Saido, Chama.

Walioonyeshwa kadi: Sawadogo 37′

X1: Mahamoud, Emery, Miraji, Kombo, Mulumba, Lawi, Mtenje, Konfor (Aboubakar 89′) Amza (Maabad 80′) Gerrard (Lokombi 80′), Enock (Yusuph 80′)

Walioonyeshwa kadi: Hakuna.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER