Tumeshusha Straika kutoka Ivory Coast

Tumepata saini ya mshambuliaji Freddy Michael Kouablan raia wa Ivory Coast mwenye miaka 26 kutoka klabu ya Green Eagles ya Zambia.

Kouablan amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi ambacho kinajipanga kwa ajili ya kurejesha ufalme wake.

Hadi sasa Freddy ndiye anaongoza kwa ufungaji kwenye ligi kuu ya Zambia kwa kuweka kambani magoli 14 na assist 4.

Usajili wa Kouablan umekuja saa chache baada ya kutangaza mshambuliaji mwingine mpya Pa Omar Jobe raia wa Gambia tuliyemsajili kutoka Zhenis FC ya Kazakhstan.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER