Tumeshusha kocha wa makipa kutoka Morocco

Katika kuboresha benchi la ufundi kuelekea msimu mpya wa ligi leo tunamtangaza Mohamed Rachid raia wa Morocco kuwa kocha wetu wa makipa.

Kabla ya kujiunga na kikosi chetu Mohamed alikuwa Kocha wa Timu ya Vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Al Ain Sports Club ya Falme za Kiarabu (UAE) huku pia akisimamia baadhi ya mechi za timu ya wakubwa.

Kocha Mohamed amefundisha timu za madaraja mbalimbali Falme za Kiarabu kwa miaka 18 tangu alipokwendwa mwaka 2004 akitokea Timu ya F.S.B inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Morocco akiwa kocha msaidizi.

Kocha Mohamed anajua kuongea kwa ufasaha lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa.

Mohamed anachukua nafasi ya Tyron Damons ambaye ameondoka klabuni baada ya kumalizika msimu uliopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER