Tumeshinda mbele ya Cambiaso

Mchezo wetu wa kirafiki wa mazoezi uliopigwa katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena dhidi ya Cambiaso Sports imemalizika kwa ushindi wa mabao 3-2.

Tulianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Cambiaso ambapo dakika ya pili Kibu Denis alitupatia bao kwanza baada ya kupokea pasi ya Pape Sakho.

Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia lango la Cambiaso ambapo Kibu tena alitupia la pili dakika ya 36 kwa kisigino akimalizia pasi iliyopigwa na Yusuf Mhilu.

Simon Msuva aliwapatia Cambiaso bao la kwanza dakika ya 40 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu kabla ya Sadio Kanoute kupiga la tatu na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili Kocha Seleman Matola aliwapumzisha Henock Inonga, Pascal Wawa, Kanoute, Gadiel Michael, Kibu, na Sakho na kuwaingiza Joash Onyango, Mzamiru Yassin, Kennedy Juma, Mohamed Hussein, Jimmyson Mwanuke na Taddeo Lwanga.

Dakika ya 78 Msuva aliwapatia Cambiaso bao la pili kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kulia.

Kikosi kilichoanza kilikuwa kama ifuatavyo

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Yusuf Mhilu (27), Sadio Kanoute (13), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (10).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER